Je hedhi ni nini? Hedhi ni mabadiliko yanayotokea katika mwili wa mwanamke wakati wa balehe, yakiashiria kupevuka kwa via vya uzazi, na utayari wa kuweza kupata ujauzito. Kutokana na mabadiliko hayo, kila mwezi mji wa uzazi hufanya matayarisho ya mimba. Yai likikutana na mbegu za kiume basi mimba hutungwa na mtoto ataweza kukuwa. Mwanamke au msichana asipopata ujauzito damu itatoka ukeni. Damu hii huitwa “hedhi”. Hedhi siyo uchafu na wala hupaswi kuona aibu inapotokea.
